HISTORIA YA FUPI YA PAROKIA YA MT PAULO MTUME Mwaka Disemba Parokia ya Mt Paulo Mtume ilifanya kilele cha maadhimisho Jubilei ya miaka ya huduma tangu kuanzishwa kwake Maadhimisho haya yaliongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu sana Jude Thadeus R waachi OFMCap Historia kiufupi Mnamo mwaka aliyekuwa Paroko wa Magomeni Padre Oswin Cap alianzisha Kigango cha Ubungo Msewe Katika kipindi hicho waamini wachache walisali chini ya mti wa mkorosho eneo ambalo kwa sasa kuna...
HISTORIA YA FUPI YA PAROKIA YA MT. PAULO MTUME
Mwaka 2023, 24 Disemba, Parokia ya Mt. Paulo Mtume ilifanya kilele cha maadhimisho Jubilei ya miaka 50 ya huduma tangu kuanzishwa kwake. Maadhimisho haya yaliongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu sana Jude Thadeus R’waachi, OFMCap.
Historia kiufupi:
Mnamo mwaka 1968 aliyekuwa Paroko wa Magomeni Padre Oswin (Cap) alianzisha Kigango cha Ubungo Msewe. Katika kipindi hicho waamini wachache walisali chini ya mti wa mkorosho, eneo ambalo kwa sasa kuna nyumba ya WAWATA hapa Ubungo Msewe. Kwa msaada wa Chifu G.P Kunambi, Balozi Richard Wambura alitoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa. Mwadhama Kardinali Lauriani Rungambwa aliwakaribisha Mapadre wa shirika la Consolata kuja kuanzisha jengo la Kanisa ambalo kwa sasa linatumika kama ukumbi mdogo wa Parokia.
Mnamo tarehe 18 Machi 1973, Ubungo Msewe ilipewa hadhi ya kuwa Parokia. Paroko wa kwanza alikuwa Padre Igino Lumetti akisaidiwa na Padre Romano Motter na mwenyekiti wa kwanza wa HW Parokia alikuwa Chifu G. P Kunambi.Ikiwa na waamini wapatao 100. Hawa walifanya kazi kubwa ya kujenga nyumba ya Mapdre. Mnamo tarehe 1 Februari 1973, Kigango cha Mavurunza walianza kupata huduma baada ya kupata Paroko mpya Mario Biestra.
Kanisa la sasa la Msewe lilianza kujengwa tarehe 9 Agosti 1976 na kutabarukiwa na Mwadhama Kadinarli Laurian Rugambwa tarehe 15 Februari 1978. Sherehe hiyo ilihudhuliwa na viongozi wa shirika la Consolata na serikali iliwakilishwa na Mwalimu Julius K. Nyerere. Mnamo tarehe 19 Julai 1978, Padre Romano Motter aliteuliwa kuwa Paroko wa Ubungo Msewe. Na msaidizi wake ni Padre Syrivesta.
Mnamo terehe 28 Desemba 1980 Kigango cha Makoka na Makabe vilitabarukiwa. Na tarehe 29 Aprili 1984, Kigango cha Mbezi Luis kilibarikiwa.
Terehe 23 Februari 1983 Padre Ricardo Ossola alikuja kama Paroko Msaidizi na hapo Kigango cha Kimara kikaanza kupata huduma.
Baruti kama Kigango kilizinduliwa tarehe 9 Septemba 2003, na Altare kutabarukiwa na Mhashamu Askofu Eusebius Nzigilwa mnamo tarehe 6 Julai 2012. Kigango cha Baruti kilitangazwa na Baba Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuwa Parokia Teule mnamo tarehe 6 Januari 2017. Mnamo tarehe 7 Julai 2018, Baruti ilitangazwa na Baba Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuwa Parokia kamili (Parokia ya Mt. Yahane XXIII) na Paroko wake wa Kwanza ni Padre Gervas Lyimo kuanzia Sept 2018.
Ifuatayo sasa ni jedwali ya ufupisho wa wahudumu (mapadre) waliokuwa maparoko na wasaidizi wao tangu parochial ikiwa changa hadi ilikofikia sasa hivi:
Hapo awali, Parokia ya Ubungo Msewe ilianza kama kigango kilichokuwa chini ya Paroko Pd. Oswin, Cap. mwaka 1968. Baada ya hapo, mwaka 1973 Paroko alikuwa Pd. Iginio Lumetti, imc, akisaidiwa na Pd. Romano Motter. Mwaka 1976, Paroko alikuwa Mario Biestra na msaidizi wake akiendelea kuwa Pd. Romano Motter. Mnamo mwaka 1978, Pd. Romano Motter alihudumu kama Paroko peke yake. Kufikia mwaka 1986, huduma za kichungaji ziliendeshwa na Pd. Luciano Scassia akiwa Paroko, akisaidiwa na mapadre Ricardo Ossola, Alois Cossato, na Lucio Abrami (wote wa imc). Miaka ya 1996 hadi 1999, Paroko alikuwa Pd. Lucio Abrami, imc, huku Paroko Msaidizi akiwa Pd. Alois Accossato, imc. Kuanzia 1999 hadi 2002, Paroko alikuwa Pd. Alois Accossato, imc, akisaidiwa na Pd. Jacobo Bakaneli na Pd. Piero Cravero, imc. Miaka ya 2002 hadi 2012, Paroko alikuwa Pd. Piero Cravero, imc, akisaidiwa na Pd. Peter Lumiri, Pd. Steven Silu, Pd. Memo, Pd. Angelo Parola, Pd. Atana, na baadaye Pd. Casimiro Torres. Kuanzia 2012 hadi 2015, Paroko alikuwa Pd. Dieudonné Ambinikosi, imc, akisaidiwa na Pd. Casimiro Torres. Miaka ya 2015 hadi 2020, Paroko alikuwa Pd. Casimiro Torres, imc, akisaidiwa na Pd. Angelous na Pd. Emmanuel Bwanamdogo; kati ya mwaka 2015 hadi 2017 walikuwepo pia mapadre Gervas Lyimo na André Nzuzi. Kuanzia mwaka 2020 hadi 2023, Paroko alikuwa Pd. Luke Nyachio, imc, akisaidiwa na Pd. Francesco Bernardi. Tangu mwaka 2023 hadi sasa, Paroko wa Parokia ya Ubungo Msewe ni Pd. Gerald Mulili.
Parokia ya Ubungo Msewe kwa sasa ina kigango kimoja tu kinachoitwa Mwenye Heri Sista Irene Stefani Golani, ambacho kilizinduliwa tarehe 28 Agosti 2011. Kufikia mwaka 2021, waamini walikuwa wanaendelea kuboresha mazingira yake. Parokia ina jumla ya Kanda tano (5) na Jumuiya Ndogondogo 39, zenye waamini wapatao 3,598 kutoka familia 814, kwa mujibu wa takwimu za sensa ya Wakatoliki ya mwaka 2016. Aidha, mnamo tarehe 12 Mei 2002, Masista wa Moyo Safi wa Bikira Maria kutoka India walifika na kwa sasa wanaendesha huduma za hospitali na shule ya msingi.